Pages

Showing posts with label Afande Sele The King. Show all posts
Showing posts with label Afande Sele The King. Show all posts

Tuesday, 24 April 2012

HAPPY BIRTHDAY AFANDE SELE 'THE KING'.

Haya ndo maneno ya Afande Sele kutoka kwenye ukurasa wake wa Facebook

Na sisi wanafamilia tunapenda kukutakia siku njema na Mwenyezi Mungu akubariki.

Friday, 6 April 2012

AFANDE SELE AFUNGUKA NA KUZUNGUMZIA SAKATA LILIOMKUTA HIVI KARIBUNI MJINI MOROGORO.


Afande Sele The King
---
Ndugu zangu ambao ni mashabiki wangu!!

Juzi wakati nimerejea kutoka Tanga, majira ya jioni ndugu zangu Ballet Wallet(mtupori) , Adam Lumbe na Twenty Percent (20%) walitoka na gari yangu, kwa bahati nzuri au mbaya wakapita maeneo ya NMB hapa Morogoro, wakapaki gari kwa haraka kwa kuwa Adam Lumbe alimuona kijana ambae alimtapeli katika mauziano ya pikipiki, likatokea zogo!! 

Polisi waliokuwa Lindo pale Bank wakaja kuizuia gari na pia wakawaweka chini ya Ulinzi Ballet Wallet na Adam Lumbe, licha ya maelezo waliyowapa hawakuwaelewa, 20% akataka kuchukua gari wakamkatalia, ikabidi akodi pikipiki aje nyumbani kunifuata nikafuate gari, nimefika pale Bank polisi wakakataa kunipa gari ili niende kituo kikubwa cha polisi kuwawekea dhamana ndugu zangu kwa kuwa muda huo Ballet na Adam walikua washapelekwa kituoni.

Kilichotokea baada ya hapo nilielezwa nisubiri gari ya doria nipewe Eskoti mpaka polisi lakini baada ya kufika gari ya doria wakiwa na wanamgambo wa manispaa walituvamia na kuanza kutupiga marungu na kutujerehi, wananchi ambao ni kama ndugu zangu wanamorogoro wakasogea eneo la tukio.

Polisi wakafyatua risasi hewani kuwasambaratisha tukapelekwa Polisi kituoni, pale hatukuchukuliwa maelezo haraka, baadae tukatoa maelezo baada ya wale mabwana wadogo askari kupata amri toka kwa wakubwa wao!! Jana (juzi) tukafikishwa mahakamani tukakosa dhamana, tukapelekwa ngome (jail) tukiwa kama mahabusu, leo  (jana) kwa bahati nzuri tumepata dhamana, na tumeweka wanasheria makini kusimamia HAKI yetu. 

Si kweli hata kidogo kuwa kwenye gari yangu kulikua na silaha za kijadi kwa lengo la kumdhuru mtu, walikuta fimbo yangu ile ya Mfalme wa rhyemes na kisu au kama panga ambao ni kitu cha kawaida kuwa nacho kwenye gari, na si kweli hata kidogo kuwa Ballet alikua kavaa kic..p* tu. 

Ndugu zangu wapendwa watanzania wenzangu,na mashabiki wetu kiukweli hali za jela na selo zetu ni mbaya mazingira mabovu ndugu zetu wanateseka. Nilitumia muda mchache niliokua kuwa kule kuwafariji na kuwapa moyo ingawa nilienda kwa Matatizo, na muda huu nipo hapa Nyumbani Misufini na Twenty Percent na Ballet pamoja na ndugu wengine! 

Tumechinja Mbuzi kama Sadaka au dhabihu kwa Mungu na kuchoma, kuelekeza moshi kwake kama ishara ya kumpenda na kushukuru kwa yote!! mwisho tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wote kwa usumbufu mulioupata. 

ASANTENI KWA FARAJA ZENU KWANGU WAKATI WOTE ,Ni mimi

SELEMANI ABDALLAH JUMA MUTABHAZI MSINDI .. KING OF RHYEMEZ. (AFANDE SELE).

Tuesday, 3 April 2012

MFALME WA RHYMES aka AFANDE SELE AZUA BALAA MOROGORO, RISASI ZA RINDIMA.


Mwanamuziki mkongwe nchini na mkazi wa Mjini Morogo, Suleiman Msindi maarufu kama Afande Sele ametiwa matatani mjini Morogoro jioni hii baada ya yeye na wafuasi wake kuzua rabsha katika moja ya vibanda vya Biashara vilivyopo jirani na Benki ya NMB tawi la Wami hadi Polisi kufyatua risasi angani kutuliza vurugu hizo.

Kwamujibu wa shuhuda wa tukio hilo anapasha kuwa awali vijana hao wanaodaiwa kuwa ni wapambe wa Afande Sele, walitinga wakiwa katika gari dogo na kuliegesha jirani na Benki hiyo kasha kuteremka wakiwa na mapanga mkononi jambo ambalo liliwastua askari Polisi waliokuwa lindoni katika benki hiyo.

Aidha baada ya muda mfupi huku Polisi hao wakila mingo walishanga kutokea vurugu kubwa katika moja ya vibanda hivyo, na kuwatia nguvuni vijana hao na Polisi kushikilia gari hilo kwa hatua zaidi. 

Shuhuda huyo anasema vijana hao walipokuwa chini ya ulizni ili polisi wengine waje kuwachukua pamoja na gari walilokuja nalo walidai gari ni mali ya Afande Sele hivyo wamuite aje kulichukua.

Simu ikapigwa kwa Afande Sele na alipofika alitaka achukue gari lake na hao vijana waende nalo, lakini Polisi walesema gari hilo halitatoka ndipo vurumai nyingine ikaanza katika eneo hilo.

Shuhuda napasha zaidi kuwa walifika Polisi wa doria majira ya saa kumi na mbili jioni eneo la tukio kutokana na vurugu hizo zikafyatuliwa risasi huku mawe yakirushwa jambo lililopelekea kuharibika kwa magari kadhaa.

Source na kwa habari zaidi tembelea mrokim.blogspot.co.uk

Wednesday, 28 March 2012

MWANA MOROGORO FAMILY aka MFALME WA RHYMES 'AFANDE SELE' AWEKA WAZI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE '2015'.


MFALME wa Rhymes nchini Seleman Msindi 'Afande Sele' ameweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Akizingumza hivi karibuni Sele alisema ameamua kugombea ili kuweza kuwatetea wanyonge ambao wamekosa watetezi bungeni.

Hata hivyo Msindi ambaye amekuwa akiimba nyimbo zenye 'mguso' kwa jamii zikiwemo 'Mtazamo' aliowashirikisha Solothang na Prof.J,Karata Dume na nyinginezo hakuweka wazi kuwa atasimama kwa tiketi ya chama gani.

Thursday, 8 March 2012

AFANDE SELE THE'KING AZUNGUMZIA ALONGA JUU YA MOROGORO.

Afande Sele The'King
---
Duh'wanandugu hasa wale 2liozaliwa miaka ya 70-80 Zaman kimtindo nakumbuka ilikuwa mgeni akitoka dar kuja moro anakuja na makot ya barid hata marehem mding wangu mzee msindi aliwah kwenda canada wkt nikiwa mdogo akaniletea zawad makot kibao kwa ajili ya barid la moro lkn leo mg kama dar ful joto"tabia nchi"2FANYE NINI WANANDUGU ILI MTO MOROGORO,KILAKALA,KIKUNDI,nk itiririke maji mwaka mzima kama zamani?oh'maskini morogoro mji uliozikwa vitovu vye2,GOD bles u my lovely Moro!.

*Je wewe una maoni gani kuhusu mambo haya?


Tutumie habari na matukio mbali mbali ya mji kasoro bahari kupitia barua pepe morogoromjiwetu@gmail.com