Pages

Showing posts with label Adam Kighmoa. Show all posts
Showing posts with label Adam Kighmoa. Show all posts

Tuesday, 13 March 2012

CHANGUDOA NDO ALIYE MLIZA WAZIRI.


WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (pichani) mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.

Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.

Friday, 9 March 2012

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH. ADAM KIGHOMA MALIMA AIBIWA VITU VYAKE NASHERA HOTEL MKOANI MOROGORO.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima
---
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima amibiwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.

Taarifa za kipolisi zilizopatikana kutoka mjini Morogoro  zimethibitisha kutokea wizi huo zikisema ulitokea usiku wa kuamkia leo.

Zilimkariri Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro,  Hamis Seleman taarifa zilmesema wizi umetokea wakati  waziri huyo alipokuwa  amejipumzisha  kwenye sebule ya chumba chake kwenye hoteli hiyo hadi  mida ya  10.45 ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani.

Kwa mujibu wa polisi  zimeibwa  fedha taslimu  Dola 4000 za Marekani na  Sh. milioni 1.5, pete mbili za silva zenye thamani ya sh. milioni 2, simu zenye thamani ya sh. milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya sh. 50,000, laptop mbili zenye thamani ya sh. milioni 5.6, taperecorder na headphone vyote vya sh. milioni moja.

Polisi wanasema dirisha la aluminium la chumba cha hoteli alimokuwa Malima limekutwa limevunjwa kwa kitu kigumu.

Habari zinasema nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo nje na ndani ya chumba jambo linaloashiria kuwa ni za mwizi.

Kufuatia wizi huo, walinzi watatu wa hotel hiyo wanashikiliwa na polisi huku taarufa zilizopatikana baadaye tukiandaa kurusha ripoti hii zikisema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa vimepatikana, ingawa havikutajwa.
---