Pages

Showing posts with label Vijana. Show all posts
Showing posts with label Vijana. Show all posts

Wednesday, 14 March 2012

VIJANA WAJIINGIZA KWENYE MAKUNDI YA MAUAJI KUTOKANA NA UKOSEKANAJI WA AJIRA.


KUKOSEKANA kwa ajira za vijana kumetajwa kuwa moja ya sababu za kundi hilo kujiingiza katika makundi mabaya ikiwamo yanatoteleza mauji ya vikongwe hasa wanawake nchini.


Mwenyekiti mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Consern For The Elderly Tanzania (COEL) Jamaton Magodi alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mwezi mmoja ya ujasiriamali, Usindikaji na uandishi wa habari kwa  wanachama wa shirika hilo kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Kagera yanayoendelea mjini Morogoro ambapo alisema kuwa ajira ni muhimu kwa vijana kwa kuwa wao ndiyo tegemeo la taifa.



Alisema kuwa mauaji ya vikongwe yanatokana na sababu mbalimbali zikiwamo mazingira mabovu ya malezi yasiyozingatia maadili ya taifa, kukosekana kwa ajira na rushwa na kuiomba Serikali  kushirikiana na shirika hilo katika kutoa elimu kwa wanajamii maeneo mbalimbali nchini kuhusu maadili mema.