Pages

Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Tuesday, 24 April 2012

DEREVA WA ‘BODABODA’ AUAWA KIKATLI NA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE SHAMBA LA MKONGE MAENEO YA KINGURUWILA.

 Mwili wa marehemu Omar ulivyokutwa maeneo ya Tungi.
 Gari la polisi lililokuja kuuchukua mwili.
Wananchi waliohuzunishwa na kifo cha Moro.
---
KASI ya madereva wa pikipiki za biashara ya kusafirisha watu zinazojulikana kama 'Bodaboda' kuuawa kikatili inashika kasi mkoani Morogoro ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Omari ameuawa na kutupwa kwenye mashamba ya mkonge ya Kinguruwila mkoani Morogoro jirani na kiwanda cha kusindika tumbaku cha Dimon.
 Wakizungumza na mtandao huu, baadhi ya madereva wenzake walisema majuzi dereva mwenzao alipigiwa simu na wateja zake awafuste maeneo ya Tungi na tangu aende huko  hajaonekana hadi mwilili wake ulipookotwa.
                          
PICHA NA HABARI DUNSTAN SHEKIDELE, GPL,  MOROGORO

Friday, 9 March 2012

WAZIRI MATHAYO ATOA MATUMAINI KWA WANANCHI WA MOROGORO.

 Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo - Dk. Mathayo David Mathayo
---
Na Mwandishi wetu,

WANANCHI hapa nchini huenda wakaondokana na kero ya ukosefu wa maeneo ya uzalishaji,huduma za jamii,kilimo na makazi baada ya serikali kutangaza dhamira yake ya kuyarejesha mikononi mwa wananchi maeneo yote yaliyotelekezwa na kushindwa kuendeleza na wamiliki wake.

Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dk David Mathayo amesema wilayani Mvomero mkoani hapa kwamba maeneo hayo yatarejeshwa mikononi mwa wananchi kwa kuzingatia sheria za ardhi na uwekezaji ili kuinua uchumi wa mwanachi,serikali na kuepusha migogoro ya ardhi iliyojitokeza mara kwa mara katika jamii ya watanzania.

Waziri Mathayo alibainisha kuwa uamuzi huo unakuja baada ya serikali kubaini maeneo mengi yametelekezwa na watu na kuamsha migogoro baina ya jamii ya wakulima na wafugaji na mipaka ya vijiji.

Alisema wananchi wa wilaya ya Mvomero,Kilosa na kilombero mkoani Morogoro wananchi wamekuwa wakilalamika kukosa maeneo ya ardhi ya kilimo na ufugaji kutokana na maeneo mengi kumilikiwa na wachache ambao hadi sasa wameshindwa kuyaendeleza kulingana na makusudio waliyoombea.

Aidha alisema kuwa wakati umefika kwa serikali kutengua umiliki wa ardhi kwa wawekezaji hao na kuwarudishia wananchi walio wengi amabo kwa kiasi kikubwa wanakumbwa na tatizo la kukosa ardhi .

Aliwataka wawekezaji kutambua kuwa maeneo wanayopewa na serikali wanapaswa kuyaendeleza nakuwa serikali ilipotoa maeneo hayo kwao ilikusudia yaendelezwe katika shughuli za uzalishaji mali na kuongeza uchumi wa nchi.