Pages

Showing posts with label Habari za Michezo na Burudani. Show all posts
Showing posts with label Habari za Michezo na Burudani. Show all posts

Tuesday, 24 April 2012

POLISI MORO YAINGIA LIGI KUU YA VODACOM, YAKABIDHIWA KOMBE.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera (kulia) akimkabidhi kombe nanodha wa timu ya Polisi Moro, Imani Mapunda, baada ya kushika nafasi ya kwanza katika Ligi Daraja la Kwanza ngazi ya kitaifa hatua ya Tisa Bora baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 20.  Mgambo Shooting Stars ya mkoani Tanga ni ya pili kwa pointi 15 na Prisons ya Mbeya ni ya tatu baada kwa  pointi 14.  Timu hizo zitaingia Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphin Chialo (mwanamke mwenye miwani katikati), akiwa na kombe la ushindi baada ya kukabidhiwa na nahodha wa timu hiyo.

PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO

Sunday, 15 April 2012

PICHA KUTOKA KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2012.

 Ma Mc Millard Ayo na Vanessa Mdee
 Mpoki akifanya vitu vyake kusema ukweli alichangamsha sana
 Vijana wa THT wakikamua
THT si mchezo

 Wanamitindo Khadija Mwanamboka na Ally Remptula wakimkabidhi tuzo msanii ya wimbo bora wa reggae kundi la Warrior from the East wa  jijini Arusha.
Taji Liundi (kushoto) akishuhudia msanii wa muziki wa kizazi kipya Queen Darleen akifurahia kupokea tuzo ya wimbo bora wa ragga/dance hall na mwanadada Abby 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Queen Darleen akishukuru kupokea tuzo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya chenye vionjo vya asili A.T akipokea tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu aliyokabidhiwa na Shelukindo na Angela Damas. 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya chenye vionjo vya asili A.T akishukuru mara baada ya kupoea wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu. 



 Komandoo Hamza Kalala (kushoto) akishuhudia Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akipokea tuzo ya wimbo wa kiswahili  (bendi) uitwao Dunia Daraja aliyokabidhiwa na Shamim Mwasha.
Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akipokea tuzo ya wimbo wa kiswahili  (bendi) uitwao Dunia Daraja.

 Msanii Diamond aliye nyakuwa tuzo 3 jana usiku akiwa katika pose na mama yake mzazi na mshikaji wake
 King Majuto akiwa kazini
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) Nassib Abdul a.k.a Diamond ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award 2012, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo nimeibuka  na tuzo tatu”,alisema.Tuzo hizo ni ( Mtunzi Bora wa nyimbo,tuzo ya video bora ya Mwaka –moyo wangu na tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume.
 Muigizaji/mchekeshaji Mahiri wa kikundi cha Vuvuzela Entertainment,Evans Bukuku akimkabidhi tuzo yake msanii Diamond,ya video bora ya mwaka.
 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora  Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi.
 Mkali wa hip hop Tanzania,Chid Benz akimkabidhi tuzo nyingine msanii Diamond ya mtumbuizaji bora wa kiume.
 Mashabiki wa Diamond akiwemo mama yake na Professor Jay wakishangilia tuzo yake

 Malkia wa mipasho akikamua na mabinti zake
 JE NI KWELI HIZI TUZO HAZITUHUSU MOROGORO?

Picha kwa hisani ya Kajunason Blog na Michuzijr Blog

Friday, 6 April 2012

AFANDE SELE AFUNGUKA NA KUZUNGUMZIA SAKATA LILIOMKUTA HIVI KARIBUNI MJINI MOROGORO.


Afande Sele The King
---
Ndugu zangu ambao ni mashabiki wangu!!

Juzi wakati nimerejea kutoka Tanga, majira ya jioni ndugu zangu Ballet Wallet(mtupori) , Adam Lumbe na Twenty Percent (20%) walitoka na gari yangu, kwa bahati nzuri au mbaya wakapita maeneo ya NMB hapa Morogoro, wakapaki gari kwa haraka kwa kuwa Adam Lumbe alimuona kijana ambae alimtapeli katika mauziano ya pikipiki, likatokea zogo!! 

Polisi waliokuwa Lindo pale Bank wakaja kuizuia gari na pia wakawaweka chini ya Ulinzi Ballet Wallet na Adam Lumbe, licha ya maelezo waliyowapa hawakuwaelewa, 20% akataka kuchukua gari wakamkatalia, ikabidi akodi pikipiki aje nyumbani kunifuata nikafuate gari, nimefika pale Bank polisi wakakataa kunipa gari ili niende kituo kikubwa cha polisi kuwawekea dhamana ndugu zangu kwa kuwa muda huo Ballet na Adam walikua washapelekwa kituoni.

Kilichotokea baada ya hapo nilielezwa nisubiri gari ya doria nipewe Eskoti mpaka polisi lakini baada ya kufika gari ya doria wakiwa na wanamgambo wa manispaa walituvamia na kuanza kutupiga marungu na kutujerehi, wananchi ambao ni kama ndugu zangu wanamorogoro wakasogea eneo la tukio.

Polisi wakafyatua risasi hewani kuwasambaratisha tukapelekwa Polisi kituoni, pale hatukuchukuliwa maelezo haraka, baadae tukatoa maelezo baada ya wale mabwana wadogo askari kupata amri toka kwa wakubwa wao!! Jana (juzi) tukafikishwa mahakamani tukakosa dhamana, tukapelekwa ngome (jail) tukiwa kama mahabusu, leo  (jana) kwa bahati nzuri tumepata dhamana, na tumeweka wanasheria makini kusimamia HAKI yetu. 

Si kweli hata kidogo kuwa kwenye gari yangu kulikua na silaha za kijadi kwa lengo la kumdhuru mtu, walikuta fimbo yangu ile ya Mfalme wa rhyemes na kisu au kama panga ambao ni kitu cha kawaida kuwa nacho kwenye gari, na si kweli hata kidogo kuwa Ballet alikua kavaa kic..p* tu. 

Ndugu zangu wapendwa watanzania wenzangu,na mashabiki wetu kiukweli hali za jela na selo zetu ni mbaya mazingira mabovu ndugu zetu wanateseka. Nilitumia muda mchache niliokua kuwa kule kuwafariji na kuwapa moyo ingawa nilienda kwa Matatizo, na muda huu nipo hapa Nyumbani Misufini na Twenty Percent na Ballet pamoja na ndugu wengine! 

Tumechinja Mbuzi kama Sadaka au dhabihu kwa Mungu na kuchoma, kuelekeza moshi kwake kama ishara ya kumpenda na kushukuru kwa yote!! mwisho tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wote kwa usumbufu mulioupata. 

ASANTENI KWA FARAJA ZENU KWANGU WAKATI WOTE ,Ni mimi

SELEMANI ABDALLAH JUMA MUTABHAZI MSINDI .. KING OF RHYEMEZ. (AFANDE SELE).

Thursday, 5 April 2012

AFANDE SELE NA 20% WAPATA DHAMANA.

NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO

WASANII nyota wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Seleman Msindi   ‘Afande Sele’ na Abbas  Hamis ‘20 Per Cent’  waliokuwa mahabusu toka juzi wakikabiliwa na kesi tano ikiwemo moja ya kushambulia,  wametoka nje baada ya kupata wadhamini mchana huu kufuatia kesi zao zilizokuwa zikisikilizwa katika mahakama ya Mwanzo Mazimbu, Mkoani Morogoro,  kuahirishwa hadi Aprili 10 na Aprili 12 mwaka huu.

Akizungumza na mtandao huu nje ya mahakama muda mfupi baada ya kupata dhamana, Afande Sele alilitupia lawama jeshi la polisi akidai hivi sasa limekithiri kwa kuwabambikizia watu kesi,

Katika hatua nyingine, mwanamuziki huyo  alimueleza mwandishi wetu nia yake ya kugombea ubunge Jimbo la Morogoro katika uchaguzi wa 2015  ili kupambana na kero nyingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ikiwemo kero hiyo ya jeshi la polisi.

Kwa upande  20 Per Cent, yeye aliwashukuru wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa kuwaunga mkono na kuwataka polisi wasicheze na nguvu ya umma.

                                

Thursday, 15 March 2012

MOROGORO WAFANYA KWELI UENYEJI LIGI DARAJA LA KWANZA.


CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kimetuma kiasi cha Sh milioni 10 
kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya kulipa Sh milioni 25 ili kuwa mwenyeji wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza zinazotarajia kuanza Machi 31. 

Katibu Mkuu wa MRFA, Hamis Semka, amesema mjini hapa kuwa Mkoa wa Morogoro 
umetuma kiasi cha Sh milioni 10 na kilichobakia kitakamilishwa ndani ya muda uliopangwa ikiwa ni sehemu ya kukamilisha masharti ya TFF baada ya kutuma maombi yao. 

Lakini alisema Mkoa wa Morogoro mbali na kukamilisha kiwango cha fedha, pia una mazingira mazuri ya kuwezesha kuchezwa kwa fainali hizo bila kuwa na matatizo yoyote hasa kulingana na historia ya kuwa Mkoa wa Kimichezo. 

Kwa mujibu wa TFF , baadhi ya mikoa ambayo imeshatuma maombi ya kuwa mwenyeji wa 
fainali hizo ni Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ruvuma na Tabora. 

Hata hivyo, Kamati ya Ligi itatangaza kituo cha fainali hizo baada ya Machi 15 mwaka huu 
ambayo ni siku ya mwisho kupokea maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa. 

Timu zilizofuzu kucheza hatua ya fainali kutoka kundi A ni Polisi ya Dar es Salaam, Mgambo 
Shooting ya Tanga na Transit Camp ya Dar es Salaam, Kundi B ni Mbeya City Council, Mlale 
JKT ya Ruvuma na Tanzania Prisons ya Mbeya wakati Kundi C ni Polisi ya Tabora, Polisi ya 
Morogoro na Rhino Rangers ya Tabora.