Pages

Thursday, 15 March 2012

SEREKALI KUFUTA LESENI ZA UCHIMABjI MADINI.

Naibu waziri wa Nishati na Mdini Mh. Adam Malima
---
WIZARA ya Nishati na Madini imesema, njia moja wapo ya kuondoa migogoro kwenye sekta ya Madini ni kutathimini upya leseni ambazo zimetolewa kiholela kwa lengo la kubaini ‘madalali’. 

Hatua hiyo inatarajia kuanza kutekelezwa wakati wowote kuanzia sasa kwa kutumia wataalamu wake. 

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima wakati akizungumzia migogoro katika sekta hiyo inayogusa watu waliopewa maeneo makubwa ya kufanya utafiti na uchimbaji kisha wakashindwa kutimiza masharti kwa muda mrefu. 

Naibu waziri huyo alisema hoja ya kuzipitia upya leseni zote zilizotolewa na Maofisa wa Madini wa Mikoa na Kanda kwa wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo ambazo zimeshindwa kufanya kazi kulingana na masharti ya uendeshaji wa Sekta ya uchimbaji wa madini nchini na hivyo kusababisha migogoro ya kimaslahi baina ya wananchi na wenye madini. 

Naibu Waziri huyo, alitoa msimamo wa Wizara yake tarehe 7 march 2012 mjini hapa wakati akizungunza na Wadau wa Sekta ya Madini wa Mkoa wa Morogoro, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, baada ya kutembelea Tarafa ya Mkuyuni na Matombo ambazo baadhi ya vijiji vyake kuna shughuli za uchimbaji wa madini ya aina mbalimbali. 

“Tatizo la madini kwa Mkoa wa Morogoro si la leo, bali ni la siku nyingi na yana sura nyingi, yapo matatizo Kilosa, Mahenge na Morogoro vijijini, yapo ya sura ya wachimbaji, mfumo wenyewe na kuanzia sasa Serikali inayatafutia majawabu ya kudumu,” alisema Naibu Waziri wa Madini. 



Alisema Wizara inatarajia kuzipitia upya leseni zilizotolewa kwa wachimbaji wote zikiwemo za kufanyia utafiti na uchimbaji wenyewe na itakapobainika wameshindwa kutimiza masharti watanyang’anywa na maeneo hayo na kutolewa upya kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa wenye nia ya kuendeleza uchimbaji wa madini. 

“Yapo maeneo ambayo wachimbaji wadogo hawatakuwa na uwezo wao wenyewe wa kuchimba, madini yapo chini meta 300, hapa panahitajika mwekezaji mkubwa atakayeingia ubia wa kisheria na mchimbaji mdogo wenye eneo analomiliki kisheria na eneo,“ alisema Naibu Waziri. 

Kwa upande wao baadhi ya wachimbaji wadogo wenye leseni wa Mkoa wa Morogoro akiwemo Katibu wa Wachimbaji madini Wilaya ya Ulanga, Christosom Msakamba alisema , wachimbaji wadogo wamekuwa wakionewa hata haki na sheria ikiwaagukia upande wao dhidi ya wawezekaji wakubwa. 

Naye Yahaya Mkude mchimbaji mdogo wa dhahabu na rubi eneo la Matombo, alishauri utaratibu wa zamani wa Maofisa Madini kwenda kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu sheria , mazingira na masoko urejeshwe upya ili wachimbaji wanufaika na rasilimali zao. 

Awali, Kaimu Ofisa wa Madini wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi, Lucy Kimaro, alisema Mkoa una jumla ya leseni 2,289 ambapo zinazofanyakazi hadi sasa ni 100 na nyingine hazifanyi kazi, wakati leseni 450 wamiliki wake hawaonekani kabisa.

No comments: