Pages

Tuesday, 15 May 2012

TALLY FASHION (TZ).


Friday, 4 May 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WAPYA LEO.


ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI



1. OFISI YA RAIS


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,


2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,


3. OFISI YA WAZIRI MKUU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,




4. WIZARA


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,


5. NAIBU MAWAZIRI


OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI


6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,


7. OFISI YA WAZIRI MKUU


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,


8. WIZARA MBALIMBALI


Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Tuesday, 24 April 2012

POLISI MORO YAINGIA LIGI KUU YA VODACOM, YAKABIDHIWA KOMBE.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera (kulia) akimkabidhi kombe nanodha wa timu ya Polisi Moro, Imani Mapunda, baada ya kushika nafasi ya kwanza katika Ligi Daraja la Kwanza ngazi ya kitaifa hatua ya Tisa Bora baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 20.  Mgambo Shooting Stars ya mkoani Tanga ni ya pili kwa pointi 15 na Prisons ya Mbeya ni ya tatu baada kwa  pointi 14.  Timu hizo zitaingia Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphin Chialo (mwanamke mwenye miwani katikati), akiwa na kombe la ushindi baada ya kukabidhiwa na nahodha wa timu hiyo.

PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO

DEREVA WA ‘BODABODA’ AUAWA KIKATLI NA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE SHAMBA LA MKONGE MAENEO YA KINGURUWILA.

 Mwili wa marehemu Omar ulivyokutwa maeneo ya Tungi.
 Gari la polisi lililokuja kuuchukua mwili.
Wananchi waliohuzunishwa na kifo cha Moro.
---
KASI ya madereva wa pikipiki za biashara ya kusafirisha watu zinazojulikana kama 'Bodaboda' kuuawa kikatili inashika kasi mkoani Morogoro ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Omari ameuawa na kutupwa kwenye mashamba ya mkonge ya Kinguruwila mkoani Morogoro jirani na kiwanda cha kusindika tumbaku cha Dimon.
 Wakizungumza na mtandao huu, baadhi ya madereva wenzake walisema majuzi dereva mwenzao alipigiwa simu na wateja zake awafuste maeneo ya Tungi na tangu aende huko  hajaonekana hadi mwilili wake ulipookotwa.
                          
PICHA NA HABARI DUNSTAN SHEKIDELE, GPL,  MOROGORO

HAPPY BIRTHDAY AFANDE SELE 'THE KING'.

Haya ndo maneno ya Afande Sele kutoka kwenye ukurasa wake wa Facebook

Na sisi wanafamilia tunapenda kukutakia siku njema na Mwenyezi Mungu akubariki.

Sunday, 15 April 2012

PICHA KUTOKA KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2012.

 Ma Mc Millard Ayo na Vanessa Mdee
 Mpoki akifanya vitu vyake kusema ukweli alichangamsha sana
 Vijana wa THT wakikamua
THT si mchezo

 Wanamitindo Khadija Mwanamboka na Ally Remptula wakimkabidhi tuzo msanii ya wimbo bora wa reggae kundi la Warrior from the East wa  jijini Arusha.
Taji Liundi (kushoto) akishuhudia msanii wa muziki wa kizazi kipya Queen Darleen akifurahia kupokea tuzo ya wimbo bora wa ragga/dance hall na mwanadada Abby 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Queen Darleen akishukuru kupokea tuzo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya chenye vionjo vya asili A.T akipokea tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu aliyokabidhiwa na Shelukindo na Angela Damas. 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya chenye vionjo vya asili A.T akishukuru mara baada ya kupoea wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu. 



 Komandoo Hamza Kalala (kushoto) akishuhudia Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akipokea tuzo ya wimbo wa kiswahili  (bendi) uitwao Dunia Daraja aliyokabidhiwa na Shamim Mwasha.
Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akipokea tuzo ya wimbo wa kiswahili  (bendi) uitwao Dunia Daraja.

 Msanii Diamond aliye nyakuwa tuzo 3 jana usiku akiwa katika pose na mama yake mzazi na mshikaji wake
 King Majuto akiwa kazini
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) Nassib Abdul a.k.a Diamond ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award 2012, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo nimeibuka  na tuzo tatu”,alisema.Tuzo hizo ni ( Mtunzi Bora wa nyimbo,tuzo ya video bora ya Mwaka –moyo wangu na tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume.
 Muigizaji/mchekeshaji Mahiri wa kikundi cha Vuvuzela Entertainment,Evans Bukuku akimkabidhi tuzo yake msanii Diamond,ya video bora ya mwaka.
 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora  Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi.
 Mkali wa hip hop Tanzania,Chid Benz akimkabidhi tuzo nyingine msanii Diamond ya mtumbuizaji bora wa kiume.
 Mashabiki wa Diamond akiwemo mama yake na Professor Jay wakishangilia tuzo yake

 Malkia wa mipasho akikamua na mabinti zake
 JE NI KWELI HIZI TUZO HAZITUHUSU MOROGORO?

Picha kwa hisani ya Kajunason Blog na Michuzijr Blog

Saturday, 14 April 2012

WAHESHIMIWA NAPE NNAUYE NA VICKY KAMATA WAZURU MNARA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MOROGORO.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Vicky Kamata leo wamezuru Mnara wa kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Sokoine, eneo la Morogoro, ambako alifariki dunia katika ajali ya gari. Pichani, Nape na Viki wakisoma maandishi kwenye mnara huo. Walikuwa wanatoka Dodoma Kwenda Dar es Salaam.

SAIDIA KUFANIKISHA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UJANGILI KUSINI MWA AFRIKA, IKIWEMO TANZANIA.

KUMBUKUMBU YA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE MKOANI MOROGORO.

 Mtoto wa hayati Sokoine, Mhe: Namelok E. Sokoine (kulia), Naibu waziri wa Ardhi Mhe Goodlack Ole Medeye na mmoja wa wasimamizi wakishauriana mambo mbalimbali kwenye eneo la jukwaa kuu kabla ya kuwasili kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda. 
 Wananchi waliokusanyika kwenye kanisa katoliki la kumbukumbu ya hayati Sokoine wakiimba nyimbo za mila za wamaasai baada ya kukusanyika kushiriki misa hiyo. Kanisa hilo lilijengwa kwenye kijiji cha Sokoine Dakawa mkoani morogoro
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, akiteta na Mbunge wa Mvomero Amos Makala ambaye pia alihudhuria kwenye miza hiyo takatifu ya kumwombea Hayati Edward Moringe Sokoine. 
 Mtoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine, Mhe: Namelok E. Sokoine MP, kushoto na Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni Mhe: Freeman Mbowe (MP) wakifuatilia misa Takatifu ambayo iliongozwa na askofu wa kanisa hilo Jimbo la Morogoro Telesphory Mkude. Nyuma yao ni ni moja wa waandaaji kutoka Sokoine Memorial Trust, Edward Tunyon 
 Waziri Mkuu kushoto akishiriki miza takatifu ya Kumwombea Hayati Edward Moringe Sokoine, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr Mary Nagu. 
 Baadhi ya washiriki wa Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine wakishiriki katika Ibada hiyo kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro.
 Mtoto wa hayati Sokoine, Mhe: Namelok E. Sokoine, akisema neno la shukurani baada ya kufanyika misa takatifu katika kanisa hilo. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward Lowassa katika Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu,  Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine, Morogoro jana. Watatu Kushoto ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude baada ya Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye kanisa katoliki, Kigango cha Wami Sokoine jana. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watatu kulia ni Binti wa Marehemu Soine, Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum. 
 Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhasham Telsphor Mkude akibariki sanamu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye viwanja vya Kikagango cha Kanisa hilo katika kijiji cha Wami Sokoine , Morogoro baada ya kuongoza Ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude akiteta na Namelok Sokoine, Binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum katika ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine,Morogoro jana. 

Picha na habari kwa hisani ya Michuzi

Wednesday, 11 April 2012

TASWIRA ZA MAZISHI YA MSANII WA FILAMU MAREHEMU STEVEN KANUMBA.


  Baadhi yaa Waombolezaji wa msiba wa Steven Charles Kanumba wakiwasili kwenye Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam mchana huu kwa tendo la kuuhifadhi mwili wa Marehemu katika nyumba yake ya Milele

 Mwili wa marehemu kabla ya kuingizwa kaburini
 Mama mzazi wa Steven Charles Kanumba akiaga mwili wa mwanae makaburini Kinondoni baada ya zoezi hili kushindikana pale Leaders Club kutokana na msongamano kuwa mkubwa kupita kiasi. 
 Pumzika kwa amani Kanumba
 Mama Mzazi wa Marehemu Steven Charles Kanumba akiwasili Makaburini huku akiwa ameambatana na Dada Asha Baraka.
Jeneza Lenye  Mwili wa Marehemu Steven Charles Kanumba ukwekwa kaburini 
Kaburi la marehemu Kanumba likisakafiwa 
  Dah kweli Kanumba umesimika kama mshumaa1 R.I.P we will miss you
Model Millen Magese akiwa na mashada ya maua 
 Mama mzazi wa Steven Kanumba akiweka shada la maua katika kaburi la mwanae
 Watu mpaka  kwenye miti na kwa habai zilizotufik ani kwamba kuna wengine walikuwa kwenye mti wakadondoka na kukimbizwa hospitali
Kanumba ulipendwa sana na umeliza wengi sana If only wafu wange kuwa wanarudi japo kwa dakika unge amka uone huu umati.

Picha kwa hisani ya Jestina George Blog