Pages

Friday, 16 March 2012

SOKO LETU MOROGORO MJINI.

Mji wetu wa Morogoro umebadilika siku hizi, kuna mengi yaliyo ongezeka, siku hizi kuna usafiri wa Daladala, stendi Imehamia Msamvu, pia wafanya biashara wengi wamekuja kuwekeza mjini humu.

Kuna mengineyo mengi tu ukifika utajionea, lakini kikubwa zaidi nilichokiona ni mahoteli yenye hadhi Za kimataifa. 

Kwa kweli ni kitu kizuri na tunakifuraia lakini kuna Tatizo moja ambalo labda nyie ndugu zangu hamjalistukia au kama mlishalishtukia basi hatuna budi tulijadilini.
Soko la Morogor Mjini kipindi cha mvua
---
Hivi mmewahi kufika ndani ya soko la Morogoro? Kwa kweli hili soko ndilo linalouza hivyo vyakula vinavyouzwa humo mahotelini, sasa inakuwaje mahali muhimu kama hapo kutelekezwa kiasi hiki??

Mvua ikinyesha mapaa yanavuja,barabara hazipitiki! Matakataka kila kona! Na swa la la matakataka sio ndani ya Soko tu, takataka Morogoro ni kama ugonjwa sugu!! saa hao wageninaowchange na mahoteli ya kifahari msiwajengee na soko lilinganalo na hadhi ya hizo hoteli?

Soko Kuu la Morogoro 1908

1 comment:

Anonymous said...

Kweli bhana... Yaani hapo mmegusa sana Manispaa kazi kukusanya kodi tui!!!