Pages

Tuesday, 10 April 2012

ABOOD ATOA USAFIRI WA BURE KWA WAPENZI WA KANUMBA KWENDA KUMUAGA LAKINI WAAMBULIA PATUPU.

Ujumbe hapo kwenye bus: Morogoro,We Love You Kanumba.

ABOOD mmetisha & thank u for providing free buses to the people of Morogoro so as they could pay their last respect's to the late Steven Kanumba! Yaani amegawa mabasi special kutoka mikoani, ths shows how great Kanumba was.

---

BAADHI ya wakazi wa Morogoro waliofika hapo walilalamikia kushindwa kutoa heshima zao licha ya kukodi basi la Kampuni ya Abood kutoka Morogoro kuja Dar es Salaam.

“Tumekuja hapa kutoka Morogoro, tumesikitishwa na hali ilivyo hapa, mara kumi wangepeleka Uwanja wa Taifa kwenye nafasi na kila mmoja akatoa heshima zake kwa mpangilio kuliko hapa,” alisikika mmoja wa abiria aliyekuwa ameegemea basi hilo.

Alielezea kushangazwa na Kamati ya Maandalizi kuwa, imeshindwa kuweka utaratibu licha ya kufahamu kuwa watu watakuwa wengi ndiyo maana walipeleka Leaders.

Naye Meneja Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye, alisema kama ungeandaliwa utaratibu hasa wa kuaga, kila mmoja angeweza kutoa heshima zake kwa marehemu.

*Msalaba mwekundu waelemewa
Wafanyakazi waliokuwa wanatoa huduma ya kwanza walielemewa na wingi wa watu waliokuwa wakizirai kutokana na sababu mbalimbali.

Timu ya waandishi wetu ilibaini waliokuwa wakizirai ni kutokana na kusimama muda mrefu wakati wengine walikuwa wakishindwa kuhimili msongamano.

Mhudumu mmoja wa Msalaba Mwekundu, aliwaeleza waandishi kuwa takriban watu 120 walizirai na kupatiwa huduma ya kwanza na kwamba, waliokuwa na hali mbaya walikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
“Wengi tumewakimbiza Mwananyamala, hali zao siyo nzuri kwani walikuwa wamepoteza fahamu na zaidi ni wanawake,” alisema mhudumu huyo. 

na Licha ya Msalaba Mwekundu, taasisi mbalimbali zilipeleka magari ya huduma ya kwanza. Taasisi hizo ni Hospitali ya Mwananyamala, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Ndege Medics zilikuwa na kazi ya kuchukua waliozirai na kuwakimbiza hospitali.

Wakati mwili ukipotolewa viwanja vya Leaders, ving'ora vya magari hayo vilikuwa vikisikika pamoja na magari mbalimbali yaliyojitolea kuwakimbiza watu hao hospitali.

*Magari mawili ya mazishi 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kampuni ya kushughulikia mazishi iliyokuwa ikihudumia kubeba mwili wa Kanumba ya Nuru Funeral Service ilileta gari la akiba iwapo gari hilo lingepata matatizo.

Mara kwa mara, kumekuwa na gari moja ambalo ndilo linalohusika na ubebaji mwili, gari ya ziada ya Nuru Funeral ilishuhudia ikiwa pembeni kwa ajili ya kuokoa jahazi iwapo ingetokea tatizo.

“Hawa jamaa kiboko wameleta hadi gari ya ziada,” alisikika jamaa mmoja aliyekuwa pembeni ya gari hilo lililokuwa limepaki kando ya viwanja vya Leaders kabla ya kuondoka muda mfupi baada ya lile lingine kuondoka na mwili.
Trafiki waenda ‘likizoni’
Wakati huohuo, polisi wa usalama barabarani jana walikuwa 'likizo' kukamata magari yanayoiba njia kutokana na kuleta waombolezaji kwenye msiba huo.

Kuanzia saa 3:00 asubuhi, daladala za Gongo la Mboto-Msasani, Ubungo-Msasani, na zile za Mwanannyamala-Posta na Stesheni, Temeke-Posta, Tandika-Ubungo zilikuwa zikiishia Viwanja vya Leaders ‘zikimwaga’ waombolezaji.
Hata hivyo, watu hao walishindwa kuingia ndani ya viwanja vya Leaders kutokana na msongamano mkubwa wa watu waliofika kutoa heshima za mwisho kwa Kanumba.

Katika hatua nyingine, watu walilazimika kuruka ukuta wa makaburi ya Kinondoni kuingia ndani baadaya polisi kuzuia watu kuendelea kuingia.

Wanawake kwa wanaume walishuhudiwa wakibebana kuingia ndani ya yadi ya makaburi kwa kuruka ukuta, huku wengine wakidandia miti walau kupata nafasi ya kushuhudia tukio hilo.




No comments: