Pages

Thursday, 5 April 2012

AFANDE SELE NA 20% WAPATA DHAMANA.

NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO

WASANII nyota wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Seleman Msindi   ‘Afande Sele’ na Abbas  Hamis ‘20 Per Cent’  waliokuwa mahabusu toka juzi wakikabiliwa na kesi tano ikiwemo moja ya kushambulia,  wametoka nje baada ya kupata wadhamini mchana huu kufuatia kesi zao zilizokuwa zikisikilizwa katika mahakama ya Mwanzo Mazimbu, Mkoani Morogoro,  kuahirishwa hadi Aprili 10 na Aprili 12 mwaka huu.

Akizungumza na mtandao huu nje ya mahakama muda mfupi baada ya kupata dhamana, Afande Sele alilitupia lawama jeshi la polisi akidai hivi sasa limekithiri kwa kuwabambikizia watu kesi,

Katika hatua nyingine, mwanamuziki huyo  alimueleza mwandishi wetu nia yake ya kugombea ubunge Jimbo la Morogoro katika uchaguzi wa 2015  ili kupambana na kero nyingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ikiwemo kero hiyo ya jeshi la polisi.

Kwa upande  20 Per Cent, yeye aliwashukuru wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa kuwaunga mkono na kuwataka polisi wasicheze na nguvu ya umma.

                                

No comments: