Pages

Friday, 9 March 2012

WAZIRI MATHAYO ATOA MATUMAINI KWA WANANCHI WA MOROGORO.

 Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo - Dk. Mathayo David Mathayo
---
Na Mwandishi wetu,

WANANCHI hapa nchini huenda wakaondokana na kero ya ukosefu wa maeneo ya uzalishaji,huduma za jamii,kilimo na makazi baada ya serikali kutangaza dhamira yake ya kuyarejesha mikononi mwa wananchi maeneo yote yaliyotelekezwa na kushindwa kuendeleza na wamiliki wake.

Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dk David Mathayo amesema wilayani Mvomero mkoani hapa kwamba maeneo hayo yatarejeshwa mikononi mwa wananchi kwa kuzingatia sheria za ardhi na uwekezaji ili kuinua uchumi wa mwanachi,serikali na kuepusha migogoro ya ardhi iliyojitokeza mara kwa mara katika jamii ya watanzania.

Waziri Mathayo alibainisha kuwa uamuzi huo unakuja baada ya serikali kubaini maeneo mengi yametelekezwa na watu na kuamsha migogoro baina ya jamii ya wakulima na wafugaji na mipaka ya vijiji.

Alisema wananchi wa wilaya ya Mvomero,Kilosa na kilombero mkoani Morogoro wananchi wamekuwa wakilalamika kukosa maeneo ya ardhi ya kilimo na ufugaji kutokana na maeneo mengi kumilikiwa na wachache ambao hadi sasa wameshindwa kuyaendeleza kulingana na makusudio waliyoombea.

Aidha alisema kuwa wakati umefika kwa serikali kutengua umiliki wa ardhi kwa wawekezaji hao na kuwarudishia wananchi walio wengi amabo kwa kiasi kikubwa wanakumbwa na tatizo la kukosa ardhi .

Aliwataka wawekezaji kutambua kuwa maeneo wanayopewa na serikali wanapaswa kuyaendeleza nakuwa serikali ilipotoa maeneo hayo kwao ilikusudia yaendelezwe katika shughuli za uzalishaji mali na kuongeza uchumi wa nchi.

No comments: