Pages

Thursday, 22 March 2012

JOEL BENDERA AVAA PIA ‘KOTI’ LA UKOCHA WA SOKA MORO.



Joel Bendera (mwenye suti kulia) alipoanza kuwapa mafunzo wachezaji wa Polisi Morogoro jioni.
 .....Aliendelea kuwapa mafunzo na ushauri mbalimbali hadi jioni.
BAADA ya juhudi zake za kufanikisha Mkoa wa Morogoro unakuwa mwenyeji wa fainali za ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora kitaifa,  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ambaye ana shahada mbili za ukocha wa soka, ameamua kurudia pia  utaalam wake huo mkoani mwake ili kuisaidia timu ya Polisi Morogoro iweza kupanda daraja msimu ujao.

 Bendera ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars)  na Naibu Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni alianza kazi hiyo ya kuinoa timu hiyo jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mara baada ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuutangaza mji wa Morogoro kuwa mwenyeji wa fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Machi 31 mwaka huu.

"Mimi ni mkuu wa mkoa na kitaaluma ni mwalimu wa soka.  Nina digrii mbili zilizozipata Ujerumani…. Mimi na wenzangu tumezileta fainali hizo hapa itakuwa haiingii akilini kwenye nafasi tatu sisi wenyeji tukosem" alisema Bendera na kuongeza:
"Mtakapopata nafasi ya kucheza ligi kuu hata uchumi wa maisha yenu utapanda ikiwa ni pamoja na kujulikana kuliko hapa mlipo sasa.”

Akiingia kwenye ukocha, aliwaasa wachezaji hao kwamba sumu kubwa ya mpira ni ulevi na uzinzi, na kuwakumbusha kwamba siri ya mafanikio ni juhudi uwanjani, kutii maelekezo ya mwalimu na nidhmu uwanjani.

Timu zilizofanikiwa kutinga tisa bora ni: Polisi na Transt Camp za Dar es Salaam, Mbeya City na Prisons za Mbeya, Polisi na Rhino Rangers za Tabora,  Malale JKT ya Ruvuma, Mgambo Shooting ya Tanga na wenyeji Polisi Morogoro,

No comments: