MOROGORO Municipal and Kilombero District councils have managed to stop teachers' peaceful demonstration which was to have taken place on March first this year for what the teachers said were their unsettled debts in the districts.
Morogoro Regional Teachers Union (TTU) Secretary Mr Issa Ngayama told 'Daily News on Saturday' that the payment of 303,456,560.52m/- out of 467,941,047.52m/- was deposited on February 28 this year in teachers' accounts, an act that defused their fury to demonstrate.
Mr Ngayama said the total amount owed to teachers was 356.4m/- in Morogoro Municipal and in Kilombero it was 111.5m/-. More than three quarter of the demand was fulfilled. He said there were 29 teachers in the municipals who had not been paid because their documents had some problems.
The Municipal Director called them to have the problems solved and their money would be paid because corrections had been made. Speaking over the teachers debt in Morogoro Region, TTU Chairperson Judith Sauli, said teachers' debts in the whole region was 1.6bn/-.
--------------------------------------------------------------
JUMLA ya Sh303.4 milioni zimelipwa kwa walimu na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro, kati ya Sh467.9 milioni ambazo walimu walikuwa wakidai hadi kufikia Februari 28 mwaka huu.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT), Mkoa wa Morogoro Issa Ngayama alisema hayo akibainisha kuwa katika Manispaa ya Morogoro walimu walikuwa wakidai Sh 35.4 milioni huku wilayani Kilombero walimu hao walikuwa wakidai Sh111.4 milioni.
Alifafanua kuwa hadi kufikia Febriari kumi mwaka huu Sh182.8 milioni zilikuwa zimeshalipwa katika Manispaa ya Morogoro na kubakia Sh173.5 milioni hatua ambayo ilisababisha CWT kutaka kufanya maandamano ya amani kushinikiza uongozi wa manispaa hiyo kuwalipa walimu madai yao.
Ngayama alisema kuwa katika Wilaya ya Kilombero walimu walikuwa wakidai kiasi cha Sh111.4 milioni ambapo hadi kufikia Februari 10 mwaka huu Sh 27 milioni pia zilikuwa zimeshalipwa.
Katibu huyo wa CWT alisema kutokana na walimu kutaka kuandamana katika Manispaa ya Morogoro, kiasi cha Sh173.5 milioni ziliingizwa katika akaunti zao benki na kwamba hadi Februari 28 mwaka huu walimu 73 walikuwa wameshalipwa kiasi cha Sh80.2 milioni kilichosalia kulipwa lakini akasema mchakato wa uhakiki na malipo unaendelea.
Hata hivyo alisema kuwa walimu 29 wa Manispaa ya Morogoro taarifa na vielelezo vyao vya malipo vilikuwa na dosari kadhaa hivyo, Februari 28 waliitwa katika Ofisi ya Mkurugenzi ili kurekebisha dosari hizo na kwamba fedha zao kiasi cha Sh 12.7milioni zitakuwa zimepelekwa katika akaunti zao benki mwezi huu.
Hata hivyo, alisema kuwa walimu wote waliopunjwa malipo yao au kuona wameonewa katika uhakiki ambao hawazidi 30 waende kwa mkurugenzi kwa ajili ya kuondoa dosari zilizomo katika vielelezo vyao vya malipo ili malipo yao yaweze kufanyika mara moja.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Morogoro, Judith Sauli alisema katika mkoa mzima walimu walikuwa wakidai kiasi cha sh 1.6 bilioni akifafanua kuwa Manispaa ya Morogoro walimu walikuwa wakidai Sh 356.4 milioni, Wilaya ya Morogoro Sh267.8 milioni, Wilaya ya Mvomero Sh248.3 milioni, Kilosa Sh338.4 milioni, Kilombero Sh 111.4 na Ulanga Sh 254.3 milioni.
No comments:
Post a Comment