Pages

Sunday, 25 March 2012

MSAMVU KUKUSANYA SH1.6 MILLIONI.

KAMPUNI ya Msamvu properties company (T) Limited inayosimamia ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Kisasa cha Msamvu kilichopo mkoani Morogoro kinatarajia kupata Sh1.6 milioni ambazo zitatumika kuendesha miradi mbalimbali ndani ya kituo hicho.


Meneja wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho Amos Mazaba alisema fedha hizo zitapatikana baada ya  kukodisha nafasi 242 za kuweka matangazo mbalimbali ya biashara.

Mazaba alisema kampuni yake imetoa nafasi hizo na kila moja itatozwa Sh 7,000.Alisema fedha hizo zitatumika  kuendeleza miradi mbalimbali itakayokuwamo ndani ya kituo hicho.Alitaka kampuni mbalimbali mkoani Morogoro na jirani kuwekeza katika uwanja huo.


Mazaba alisema bei hiyo itasaidia kuboresha madhari ya eneo hilo na kituo hicho cha mabasi kinatarajiwa kuwa  kivutio katika nchi za afrika mashariki na kati.Ujenzi wa kituo hicho utajumuisha miundombinu mbalimbali kama vile kujengwa kwa  jengo la hoteli lenye ghorofa kumi.



Picha kwa hisani ya The Habari.Com

No comments: