Pages

Sunday, 25 March 2012

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI AJIUA.


MWANAFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro, Hemed Athuman (21), amejinyonga kw akutumia shuka baada ya kufeli mitihani.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Adolphina Chialo, alisema tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu saa 2:30 usiku nyumbani kwao, eneo la Mafiga.

Chialo alisema mwanafunzi huyo alikuwa anasoma Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro ngazi ya cheti, baada ya majibu kutoka ya kuingia semista ya pili, ilionekana hakufanya vizuri.

Kwa mujibu wa ndugu, Athuman aliacha barua ujumbe kuwa hakutendewa haki katika mitihani yake na asihusishwe mtu yeyote na kifo chake, kwani ameamua mwenyewe.

Alisema ameamua kujiua kutokana na kutotendewa haki kwenye mitihani yake huku akisema alijitahidi kusoma kwa bidii kutokana na kwamba, ndugu ndiyo waliokuwa wakimsaidia kwa sababu wazazi wake walishafariki,  lakini ameona ndoto yake haiwezi kutimia.

Hata hivyo, Chialo alisema uchunguzi zaidi wa kifo hichounaendelea.Katika lingine, mtu asiyefahamika amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.

Chialo alisema tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu saa 2:00 usiku eneo la Makunganya barabara ya Morogoro – Dodoma, gari isiyofahamika ilimgonga mtu huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.

Wakati huohuo, Martine Emilly (38), mkazi wa Kihonda, Manispaa ya Morogoro, akiwa katika pikipiki aina ya Sanlg aligongwa na gari isiyofahamika na kufariki papo hapo.

Kamanda Chialo alisema tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu saa 2:00 usiku eneo la Makunganya,  baada ya ajali hiyo kutokea mwenye gari alikimbia na polisi inaendelea na uchunguzi zaidi

No comments: