ASKOFU Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro amesifu uadilifu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimtaja kuwa ni mtu aliyeishi katika hali ya kimasikini huku akiongeza kuwa matendo yake yanapaswa kuigwa na viongozi wengine duniani.
Kutokana na sifa hizo mara baada ya kifo chake, kiongozi wa sasa wa Kanisa Katoliki Duniani, Benedict XVI aliwapendekeza Mwalimu Nyerere na Papa Yohana Paulo ambao wamefariki dunia waingie kwenye mchakato ili kuwawezesha wawe wenyeheri.
Askofu Mkude aliongoza Ibada ya kitaifa ya kumbukumbuku ya mateso ya Bwana Yesu Kristo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice la Jimbo la Morogoro.
Hivyo aliwataka Watanzania wazidi kumwombea ili aweze kutangazwa kuwa Mwenyeheri, jambo ambalo litakuwa ni ya kujivunia si tu kwa Watanzania pia na Waafrika wote, kutokana na kuzoeleka kuwa mwenyeheri ni weupe pekee.
“Mwalimu Nyerere alijitahidi kuishi katika hali ya kimasikini na matendo yake ni ya kuigwa na viongozi wengine duniani, hivyo Watanzania inabidi tumwombee ili aweze kuingia kuwa Mwenyeheri,” alisema Askofu wa Kanisa hilo.
Hata hivyo, amewashauri Watanzania wakiwemo viongozi wenye mamlaka kuachana na tabia ya kujinufaisha wao wenyewe kwa kutumia njia zisizo halali ikiwemo rushwa
No comments:
Post a Comment