Mwanamuziki mkongwe nchini na mkazi wa Mjini Morogo, Suleiman Msindi maarufu kama Afande Sele ametiwa matatani mjini Morogoro jioni hii baada ya yeye na wafuasi wake kuzua rabsha katika moja ya vibanda vya Biashara vilivyopo jirani na Benki ya NMB tawi la Wami hadi Polisi kufyatua risasi angani kutuliza vurugu hizo.
Kwamujibu wa shuhuda wa tukio hilo anapasha kuwa awali vijana hao wanaodaiwa kuwa ni wapambe wa Afande Sele, walitinga wakiwa katika gari dogo na kuliegesha jirani na Benki hiyo kasha kuteremka wakiwa na mapanga mkononi jambo ambalo liliwastua askari Polisi waliokuwa lindoni katika benki hiyo.
Aidha baada ya muda mfupi huku Polisi hao wakila mingo walishanga kutokea vurugu kubwa katika moja ya vibanda hivyo, na kuwatia nguvuni vijana hao na Polisi kushikilia gari hilo kwa hatua zaidi.
Shuhuda huyo anasema vijana hao walipokuwa chini ya ulizni ili polisi wengine waje kuwachukua pamoja na gari walilokuja nalo walidai gari ni mali ya Afande Sele hivyo wamuite aje kulichukua.
Simu ikapigwa kwa Afande Sele na alipofika alitaka achukue gari lake na hao vijana waende nalo, lakini Polisi walesema gari hilo halitatoka ndipo vurumai nyingine ikaanza katika eneo hilo.
Shuhuda napasha zaidi kuwa walifika Polisi wa doria majira ya saa kumi na mbili jioni eneo la tukio kutokana na vurugu hizo zikafyatuliwa risasi huku mawe yakirushwa jambo lililopelekea kuharibika kwa magari kadhaa.
Source na kwa habari zaidi tembelea mrokim.blogspot.co.uk
No comments:
Post a Comment