Pages

Wednesday 14 March 2012

BODI YA MISS UTALII KUKUTANA MACHI 22.


BODI ya Miss Utalii itakutana Machi 22 kutathmini mashindano ya kanda ikiwa ni pamoja na kupanga tarehe ya kufanyika kwa fainali za taifa za mashindano hayo.

Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo, alisema kikao hicho kitafanyika mjini Bagamoyo, ambapo mbali na ajenda hiyo pia kitajadili changamoto za mashindano hayo.
Chipungahelo alisema, kikao hicho kitapanga tarehe ya kufanyika mashindano ya kanda na kutangaza mkoa ambao yatafanyika mashindano hayo msimu huu.

Alitaja mikoa ambayo inapigana uenyeji ni Morogoro, Arusha, Mwanza, Dodoma, Tanga na Dar es Salaam.

"Fainali za Miss Utalii zitashirikisha warembo 78 wenye mataji ya kanda, mikoa na vyuo vikuuu.

Mashindano hayo yataonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni kutangaza utalii na utamaduni kupitia jukwaa la sanaa ya urembo.

Aliwataja wajumbe watakaoudhuria kikao hicho ni Vikas Gupta, Abubakari Omary, Dim Mbapila, Samwel Malecela, Francis Chipungahelo, George  Ntevi, Sarah Ramadhani na wanahabari wa Miss Utalii Fredy Wanjala na Kambi Mbwana.

No comments: