Pages

Wednesday, 14 March 2012

SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE YA TOA MAFUNZO KWA WAFUGAJI WA ASILI.


CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo  cha Morogoro, kimetoa mafunzo kwa wadau 65 wa mnyororo wa thamani, kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa nyama na maziwa katika mfumo wa ufugaji wa ng’ombe wa asili  wilayani  Kilosa.


Hatua hiyo inalenga katika kuwawezesha wafugaji  kuongeza pato la kaya zao na  taifa kwa jumla.Hayo yalisemwa juzi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa, Mohamed Maje, alipokuwa akifungua warsha iliyowashirikisha wadau wa sekta ya mifugo.

Maje alisema mafunzo hayo ni muhimu katika ustawi wa wadau wa mnyororo wa thamani wanaozalisha  mazao ya mifugo ikiwamo nyama na maziwa.Alisema lengo la warsha hiyo ni kutoa mafunzo ya kinadharia kuhusu mnyororo wa thamani na kuchanganua matatizo yanayowakabili katika uzalishaji wa mazao ya mifugo.

Mratibu wa mradi huo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Dk Esron Karimuribo alisema mradi unafanya utafiti shirikishi utakaodumu kwa miaka mitatu.

No comments: