Pages

Wednesday 14 March 2012

MTIBWA SUGAR YAILALMIKIA TFF.



UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umelilalamikia Shirikisho la soka nchini (TFF) kwa kuipa Simba wenyeji wa mechi baina yao.

Timu hizo zitakutana katika mechi ya Ligi Kuu Bara Jumapili ijayo mjini Morogoro, hata hivyo katika ratiba ya TFF inaonyesha kuwa, mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa na Simba ndiyo mwenyeji wa mchezo huo.


Meneja wa kikosi hicho, David Bugoya ameliambia gazeti hili kuwa: ''Tunashangaa Simba kupewa kuwa mwenyeji wa mechi hiyo.''

''Sisi ndiyo wenyeji wa mechi hiyo, kwani hata katika ratiba ya TFF inaonyesha wenyeji ni Simba na itachezwa Dar es Salaam jambo ambalo si sahihi,'' alisema Bugoya.

Akijibu madai hayo Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura amesema; ''ratiba ilikosewa, mechi itachezwa Morogoro na Mtibwa Sugar ndiyo wenyeji.''

No comments: